Sat, April 25, 2020 at 1:31 pm GMT
Hallo friends i want us to learn kiswahili especially on Vivumishi
Mifano
'Kuku yule ' mweusi ametaga mayai kumi
Askari magereza amepigwa na mfungwa
'Kaka unanipa hadithi ya kuvutia
Raia mwema amehama mtaa
Kivumishi ni neno /maneno yanayotoa taarifa ya ziada katika nomino . Kivumishi hufanya kazi ya kufafanua/kuelezea zaidi kuhusu nomino ili kupambanua/kuitofautisha nomino husika miongoni mwa nomino nyingine.
Kiwakilishi ni aina ya maneno ambayo husimama kuwakilisha nomino. Kivumishi hutoa taarifa ya ziada kuhusu nomino, kiwakilishi (endapo nomino haipo) au kivumishi chenzake (endapo kuna vivumishi zaidi ya kimoja katika tungo husika).
Mifano
Kijana yule ana tabia nzuri
Majumba kumi yamevunjika
Mawingu meusi yametanda angani
Yule mpole amesafiri
Bata mweupe ni wa jirani
Aina za vivumishi
1. Vivumishi vya sifa
2. Vivumishi vya idadi pia vya kiasi
3. Vivumishi ya kuuliza
4. Vivumishi vya kuonesha/Vivumishi vionyeshi/viashiria
5. Vivumishi vya kumiliki
6. Vivumishi vya -a unganifu
7. Vivumishi vya urejeshi
8. Vivumishi vya pekee
9. Vivumishi vya jina kwa jina /nomino
10. Vivumishi visisitizi
Inafanana kabisa na orodha ya viwakilishi, tofauti yake ni hali ya nafsi tu. Yaani, hakuna kivumishi cha nafsi.